Kampuni ya mtandao wa kijamii Facebook, mnamo Jumapili, Januari 17, ilizima ujumbe wa Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya kwa Rais Yoweri Museveni wa Uganda kwa madai kuwa ulikuwa wa kupotosha.
Ikulu ya Kenya ililazimika kufuuta ujumbe huo kufuatia onyo la Facebook, ambapo Rais Uhuru alikuwa amempongeza Museveni kwa kushinda uchaguzi wa urais nchini Uganda.
Sehemu ya ujumbe huo ilisoma, “…..Ushindi wa Yoweri Museveni kama ushahidi tosha kuwa wananchi wa Uganda wana imani na uongozi wake……,”
Huku Facebook ikitoa onyo lake, ikisema kuwa uchunguzi ulifanywa na wachunguzi huru na kubainika kuwa ujumbe huo ni feki.
Haya yanajiri huku mpinzani wa karibu wa Museveni, Robert Kyagulanyi Ssentamu, almaarufu Bobi Wine, akipinga matokeo ya uchaguzi akidai kura ziliibiwa. Bobi Wine alisema ana ushahidi ambao ataanika punde serikali itakaporejesha mtandao Jumatatu, Januari 18.
Rais Museveni mwenye umri wa miaka 76 tayari amelitumikia taifa hilo la Uganda kwa miaka 35 ambapo kwa ushindi huo wa uchaguzi wa 2021 ameongeza miaka mingine mitano ya utawala baada ya kishinda uchaguzi wa Urais,kwa kura 5,851,037 huku mpinzani wake wa karibu,Bobi Wine akipata kura 3,475,298.
Ikumbukwe kwamba Museveni ameingia madarakani tangu mwaka 1986.