Wakenya 10 waliokuwa wametengwa kwa lazima au karantini ya lazima nchini Uganda baada ya kupatikana nchini humo kinyume cha sheria kufuatia amri ya kutoingia nchini humo kama njia moja ya kuzuia kuenea zaidi kwa ugonjwa wa Covid-19 .Wameruhusiwa kuingia nchini Kenya au Nyumbani baada ya kuzuiliwa karantini kwa siku 14.
Kamishona wa kaunti ya Busia,Joseph Kanyiri, amesema 10 hao walikuwa wanazuiliwa katika shule ya msingi ya Maribira karibu na mpaka wa Kenya na Uganda,na kutoa wito kwa Wakenya haswa wavuvi kukoma kuvuka mpaka wa hizi nchi mbili ili Kuzuia visa vya kutiwa mbaroni na maafisa wa Uganda.
Aidha amesema mipaka ya Malaba na Busia imefungwa au ilifungwa hadi pale maradhi ya Covid 19 yatakapodhibitiwa .