14.6 C
Nairobi
Thursday, August 5, 2021
Kenya
206,691
Total confirmed cases
Updated on August 5, 2021 8:34 am

SARAH OBAMA, BIBI YA RAIS WA ZAMANI BARACK OBAMA AFARIKI DUNIA

Sarah Obama, bibi ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amefariki dunia katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu akiwa na miaka...
More

  Latest Posts

  7 WAFARIKI KATIKA AJALI YA BARABARANI NJORO-KENYA

  Watu 7 wapoteza maisha, 11 wajeruhiwa vibaya kwenye ajali ya barabarani Njoro nchini Kenya Ijumaa machi 5,2021 usiku.

  Watu sita walifariki dunia papo hapo,huku mmoja akifariki hospitalini akipokea matibabu na wengine kujeruhiwa vibaya wakati gari walilokuwa wakisafiria kupoteza mwelekeo na kuingia shimoni katika shamba la Muthera huko Njoro, Kaunti ya Nakuru.

  11 waliojeruhiwa walipelekwa katika hospitali ya Nakuru Level Five na 6 waliachiwa kwenda nyumbani leo.

  Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Nakuru Tito Kilonzi alisema ajali hiyo ilitokea katika makutano ya shamba hilo kubwa. “Waathiriwa walikuwa kwenye lori ambalo dereva wake alishindwa kudhibiti na kuelekea shimoni. Watu sita walipoteza maisha yao papo hapo. Saba wako katika hali mbaya na wengine wachache walipata majeraha madogo,” alisema Kilonzi.

  Aliongeza kuwa miili ya watu waliofariki dunia iliondolewa na kupelekwa katika makafani ya Chuo Kikuu cha Egerton.

  Kulingana na Patrick Njoroge ambaye alishuhudia ajali hiyo,lori hilo lilikuwa likiendeshwa kwa kasi mno wakati dereva alishindwa kulidhibiti baada ya kulipita gari lingine kwenye kona.

  Waathiriwa walikuwa wafanyikazi wa shamba ambao walikuwa wamebebwa kwenye lori hilo la kusafirisha viazi baada ya kukamilisha kazi yao ya mchana.

   

   

   

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: