19.4 C
Nairobi
Saturday, October 16, 2021
Kenya
251,669
Total confirmed cases
Updated on October 14, 2021 9:34 pm

SARAH OBAMA, BIBI YA RAIS WA ZAMANI BARACK OBAMA AFARIKI DUNIA

Sarah Obama, bibi ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amefariki dunia katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu akiwa na miaka...
More

  Latest Posts

  AFIA GESTI BAADA YA KUNYIMWA TENDO LA NDOA NA MPANGO WA KANDO (MCHEPUKO)

  Mwanaume mwenye umri wa miaka 59, amefia gesti iitwayo Urembo iliyoko Ntimaru mjini,eneo bunge la Kuria Mashariki katika Kaunti ya Migori.

  Kwa mujibu wa mwenye gesti hiyo, mwanaume huyo na mchepuko wake wa kutoka 2013 aliwasili kwenye gesti hiyo na kulipia chumba,kisha mwanaume huyo akamnunulia mchepuko wake soda na mkate na kumuacha nje akiinywa.Mwanaume akaingia chumbani ambapo alikula dawa almaarufu Viagra.

  Mchepuko alipoingia kwenye chumba hicho na kumnyima mwanaume huyo tendo la ndoa kwa kusingizia kuwa yuko kwenye siku zake za hedhi.

  Mwanaume huyo alianza kujigalagaza kitandani huku akiguna ndipo mchepuko akamuita muhudumu wa hapo na kumueleza kinachoendelea.

  Walijaribu kuokoa maisha yake kwa kumkimbiza kwenye hospitali ya kibinafsi iliyoko karibu ila kufika alikuwa ameisha fariki dunia.

  Kwa sasa mwanamke huyo ameshikiliwa na Police katika kituo cha Polisi cha Ntimaru kwa uchunguzi zaidi, amesema OCPD wa eneo hilo John Losia.

  Hata hivyo mwili wa mwanaume huyo umehifadhiwa katika hospitali ya Migori Level Four kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji kwa uchunguzi zaidi.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: