19.4 C
Nairobi
Friday, October 15, 2021
Kenya
251,669
Total confirmed cases
Updated on October 14, 2021 9:34 pm

SARAH OBAMA, BIBI YA RAIS WA ZAMANI BARACK OBAMA AFARIKI DUNIA

Sarah Obama, bibi ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amefariki dunia katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu akiwa na miaka...
More

  Latest Posts

  AFISA WA POLISI ASHINDWA KUVUMILIA KIU CHA MVINYO

  Afisa mmoja wa polisi alizua vurugu katika baa moja eneo la kibiashara la Kanyenyaini katika kaunti ya Murang’a nchini Kenya,baada ya kutishia kuwapiga risasi wauzaji.

  Inaarifiwa kwamba afisa huyo anayejulikana kama Patrick Kiptoo alikuwa akishika doria katika benki moja mjini humo wakati alizidiwa na kiu cha bia na kuingia kwenye baa moja.

  Mmiliki wa baa hiyo, Hannah Njeri alisema Kiptoo alifika katika baa hiyo akiwa na sare rasmi za kazi na bunduki yake mkononi huku akionekana mlevi tayari na aliagiza apewe kinywaji kingine ambapo Njeri alikataa kumpa na hali ikabadilika mara moja.

  Afisa huyo alizua vurugu huku akitishia kufyatua risasi iwapo hatapata kinywaji chake. Ilimbidi Njeri kuingia mafichoni akihofia maisha yake kwani afisa huyo alikuwa amekuwa mkali. Baada ya Njeri kuingia mafichoni, Kiptoo alifyatua risasi hewani kabla ya kuondoka na kurudi kazini kwenye benki alipokuwa akishika doria.

  Maafisa wengine wa polisi walifika eneo la mkasa lakini Kiptoo alikuwa ameondoka na hivyo wakamfuata mpaka kwenye benki hiyo. Walimkamata na kutwaa bunduki yao huku akipelekwa katika kituo cha Kangema ambapo alizuiliwa huku uchunguzi ukianzishwa.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: