Mwanamke mmoja amekamatwa na polisi kwa madai ya kumuua mume wake kwa kumdunga kwa kisu katika kijiji cha Twiga,Kaunti ya Trans Nzoia usiku wa kuamkia leo Machi 3,2021.
Kisa hicho cha kusikitisha, mwanamke huyo amemuua mume wake kwa kumdunga kisu kooni kufuatia mzozo wa kutokuwa na uaminifu kwa ndoa yao.
Kwa mujibu wa binamu yao, wanandoa hao wamekuwa wakizozana na kwamba juhudi zao za kuwaongelesha kwa lengo la kuwa na uelewano mzuri kwenye ndoa yao zimeonekana kugonga mwamba.
Majirani nao wameelezea jinsi watoto wa mwendezake walivyoshtushwa na tukio hilo huku damu ikiwa imetapakaa chumbani.
Naibu wa Chifu wa Kata ya Twiga mahali kisa hicho kilipotokea, Rukia Majengo amesema maafisa wa usalama wamemnusuru mwanamke huyo kutoka kwa umma uliokuwa umejawa na ghadhabu uliolenga kumuua pia.