22.8 C
Nairobi
Friday, October 15, 2021
Kenya
251,669
Total confirmed cases
Updated on October 14, 2021 9:34 pm

SARAH OBAMA, BIBI YA RAIS WA ZAMANI BARACK OBAMA AFARIKI DUNIA

Sarah Obama, bibi ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amefariki dunia katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu akiwa na miaka...
More

  Latest Posts

  ALIYEKUWA JAJI MKUU WA KENYA EVANS GICHERU AFARIKI DUNIA

  Kifo cha Gicheru kilitangazwa na Jaji Mkuu anayeondoka David Maraga Jumamosi Desemba 26,2020.

  Taarifa ya Maraga iliyotolewa Desemba 26 ilionyesha Gicheru alifariki siku ya jana(Krisimasi).

  Gicheru aliteuliwa kuwa Jaji Mkuu Kenya mwaka wa 2003 baada ya serikali ya aliyekuwa Raisi Mwai Kibaki kushika hatamu za uongozi mpaka mwaka 2011.

  Awali alihudumu kwenye uongozi wa utawala wa kimikoa kabla ya kujiunga na Idara ya Mahakama 1982 kama jaji wa Mahakama ya Rufaa.

  Amewaacha mke (Margaret Gicheru) na watoto saba.

  Kulingana na familia, walikuwa pamoja kwenye klabu cha Arbadere siku ya Alhamisi tarehe 24,mwezi wa 12,2020.alipoamua kufanya mazoezi kwa kutembea na wakamkosa.Msako mkali wa kumtafuta ukafanyika ambapo tarehe 25 (Krisimasi) alipatikana akiwa amelala kwenye kichaka na akapelekwa hospitali.

  Gicheru atakumbukwa sana kwa kumuapisha Mwai Kibaki wakati wa uchaguzi wa Urais 2007 uliozua ghasia baada ya mpinzani wake Raila Odinga kudai uliibwa.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: