Aliyekuwa mkuu wa majeshi Zimbabwe, Jenerali Luteni Douglas Nyikayaramba amefariki kutokana na matatizo ya COVID-19 Jumanne Februari 09,2021.
Jenerali Luteni mstaafu Douglas Nyikayaramba ndiye aliongoza jeshi la Zimbabwe kuipindua serikali ya Rais Robert Mugabe mwaka 2017.
Disemba 2020 Zimbabwe iliwapoteza mawaziri watatu na kuongezea idadi ya maafisa wakuu walioangamia na virusi hivyo kuwa wanne.Yeye akiwa balozi wa pili kuangamia chini ya wiki mbili kufuatia kifo cha balozi wa taifa hilo katika nchi ya Milki za Uarabuni (UAE), Jethro Ndlovu.
Mkuu huyo wa zamani wa Jeshi, alikuwa Balozi wa Zimbabwe nchini Mozambique baada ya kuteuliwa na Rais Emmerson Mnangagwa mwaka 2019.
Miongoni mwa sheria zilizowekwa na serikali ya Zimbabwe kudhibiti kuongezeka kwa maambukizi ya Covid 19 ni, serikali kufunga shughuli zote nchini humo mnamo Januari 5, Sheria ya kafyu kuanzia saa kumi na mbili jioni hadi saa kumi na mbili asubuhi inaendelea huku ndege za kimataifa zikiruhusiwa kulingana na mahitaji yaliyotolewa na Wizara ya Afya na Kila mtu lazima avalie maski katika maeneo ya umma na kudumisha umbali huku shule, hoteli na baa zote zikifungwa.
Kufikia Februari 10, 2021,Zimbabwe imethibitisha visa 34,781 vya COVID-19 na vifo 1353.