18.4 C
Nairobi
Saturday, May 8, 2021
Kenya
162,666
Total confirmed cases
Updated on May 8, 2021 10:17 am

GAVANA WA ZAMANI WA NAIROBI MIKE SONKO AACHILIWA KWA DHAMANA

Hatimaye aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko ameachiliwa kwa dhamana baada ya kuzuiliwa rumande kwa muda wa takribani mwezi mmoja. Kwa mujibu wa TUKONEWS, Sonko...
More

  Latest Posts

  ATIWA JELA MIAKA 30 KWA KUMBAKA MTOTO WAKE WA KUMZAA

  Mahakama ya Mkoa wa Singida nchini Tanzania, imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela mwanaume Hamisi Mtanda wa miaka 37 kwa kosa la ubakaji.
  Mtanda amehukumiwa kifungo hicho baada ya mahakama kumpata na kosa la kufanya mapenzi na mtoto wake wa kike, mwenye umri wa miaka 11.

  Mwanasheria wa Serikali Elizabeth Barabara, alidai kuwa mshtakiwa alitengana na mke wake, ambaye ni mama mzazi wa mtoto huyo, na hivi sasa anaishi jijini Dar es Salaam na alikwenda kumchukua mtoto huyo akiwa na umri wa miaka sita na kuanza kuishi naye. Kuanzia Julai, mwaka jana, alianza kumchokonoa kwa vidole.Kipindi hicho chote mshatakiwa aliishi na mwanae kabla ya kuanza kumwingilia kimwili mtoto ambaye ni mwanafunzi (jina la shule linahifadhiwa).

  Alidai kuwa mshtakiwa baada ya kuona sehemu za siri za mtoto zimetanuka, alikuwa akimnyemelea usiku akiwa amelala ndipo alipoanza kumwingilia kimwili na wakati akifanya unyama huo, mtoto alikuwa akipiga kelele za kuomba msaada bila mafanikio kutokana na maumivu aliyokuwa akiyapata.

  Mwanasheria huyo alidai kuwa, kutokana na mshtakiwa kukana shtaka la kutenda kosa hilo, upande wa Jamuhuri ulipeleka mashahidi sita, akiwamo daktari ambaye alithibitisha bila kuacha shaka yoyote kwamba mshtakiwa ndiye aliyemwingilia mtoto huyo.

  Kutokana na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka, mahakama ilijiridhisha kuwa mshtakiwa huyo ndiye aliyemfanyia unyama huo mtoto wa kumzaa mwenyewe.

  Kabla ya kutolewa adhabu, mshtakiwa alipewa nafasi ya kujitetea kwa kudai kuwa hakufanya unyama huo bali mtoto huyo alikuwa amefanya vitendo vya ngono na mwalimu, bila kumtaja ni mwalimu yupi.

  Akitoa hukumu, Hakimu Mkazi Mwandamizi Robert Oguda, alisema anamhukumu mshtakiwa kifungo cha miaka 30 jela, ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama za mshtakiwa huyo.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: