14.6 C
Nairobi
Thursday, August 5, 2021
Kenya
206,691
Total confirmed cases
Updated on August 5, 2021 6:33 am

SARAH OBAMA, BIBI YA RAIS WA ZAMANI BARACK OBAMA AFARIKI DUNIA

Sarah Obama, bibi ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amefariki dunia katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu akiwa na miaka...
More

  Latest Posts

  ATIWA MBARONI KWA KUSHIRIKI NGONO NA BINTI YAKE WA MIAKA 11

  Polisi wilaya ya Serengeti mkoani Mara nchini Tanzania,inamshikilia mkazi wa kitongoji cha Chamoto, Ikwabe Gibogo (58) kwa tuhuma za kumwingilia kimwili mtoto wake wa kike mwenye umri wa miaka (11).

  Mwenyekiti wa Kitongoji hicho, Marwa Nyambuge amethibitisha mtuhumiwa kukamatwa Januari 23, 2021 usiku baada ya polisi kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema na kumkuta nyumbani kwake.

  Siku ya tukio la kukamatwa kwa bwana Gibogo, maafisa wa polisi walimkuta mtuhumiwa amelala chini pamoja na mtoto huyo wote wakiwa hawajavaa nguo.
  Mmoja wa majirani amesema mtoto huyo ameingiliwa kwa muda mrefu na baada ya kujiridhisha waliamua kutoa taarifa kwa kiongozi wa kitongoji na polisi walipofika waliwapa ushirikiano.

  Joseph Magoiga, ambaye ni Mwenyekiti mstaafu wa kitongoji hicho aliliambia Mwananchi kuwa mtuhumiwa alianza kufanya ngono na mwanae mkubwa, ambaye pia alikuwa na umri chini ya miaka 18 na kumpa mimba na kuzaa naye mtoto.

  Pia taarifa za vitendo vyake hivyo vimewashtua wengi alipokutwa na watoto wawili akiwemo huyo wa kike na mwingine wa miaka (4), ambaye inadaiwa alizaa na binti yake mkubwa baada ya kuolewa ikabainika alipewa mimba na baba yake akalazimika kumpelekea mtoto wake na kutokomea mkoani Simiyu.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: