Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 30 amuua ndugu yake wa damu katika kijiji cha Gwikonge,kaunti ya Migori, nchini Kenya.
Mwanaume huyo Sagamo Nyakimu 30,amemuua nduguye Hamisi Nyakimu Gimonge mwenye umri wa miaka 33 nyumbani kwao kwa kumkatakata kwa panga.
Kwa mujibu wa OCPD wa Kuria Magharibi Cleti Kimaiyo, amesema kisa hiki kimeripotiwa na mwanakijiji aliyeshuhudia na kuongeza kwamba Hamisi ambaye ni mgonjwa wa akili alimshambulia mamake mzazi, Rebecca Nyakimu mwenye umri wa miaka 62.Mamake alikimbilia kwa nyumba ya Sagamo.Hivyo vita vikali vikaanza kati ya ndugu hao wawili ambapo Sagamo alichukua panga na kumkatakata Hamisi hadi kufa kisha kutoweka na panga hiyo.
Polisi wameanzisha msako mkali kumtafuta Sagamo.
Mwili umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Ombo Mission.