Familia yacharangwa mapanga na mkwe wao kule nchini Tanzania.
Mwandu Chalya (75) na mke wake Gigwa Kwangu (70) wakazi wa kijiji cha
Mwamasololo, wilayani Kishapu wamenusurika kufa baada kukatwa na kitu
chenye ncha kali ‘panga’ na mkwe wao ‘Mkwilima’ Masele Boniface akilipiza kisasi
kwa sababu wamekataa asirudiane na mke wake aliyetengana naye kwa kupeana
talaka mahakamani.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba amesema tukio
hilo limetokea siku ya 29 mwezi huu majira ya saa nane usiku katika kitongoji cha
N’halange, kijiji cha Mwamasololo, taarafa ya mondo, wilaya ya Kishapu.
Amesema Mwandu Chalya (75) pamoja na mke wake aitwaye Gigwa Kwangu (70)
wote wakazi wa Mwamasololo walijeruhiwa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali
sehemu mbalimbali za miili yao na mkwe wao ‘Mkwilima’ Masele Bonifce wakiwa
wamelala ndani ya nyumba yao.
ACP Debora amesema kuwa,chanzo cha tukio hili ni chuki /kulipiza kisasi baada ya
wazazi wa mke wake aitwaye Emiliana Mwandu (31) mkazi wa Mwamasololo
kumkataza kurudiana na Masele au huyo aliyewakatakata kwa panga baada ya
kutengana kwa kupeana talaka mahakamani mnamo tarehe 06/05/2019 kwa
sababu za ukatili aliokuwa akifanyiwa na mtuhumiwa kwa kupigwa hadi kupoteza
fahamu kipindi hicho 2019.
Pia amesema majeruhi wanapatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya mkoa
wa Shinyanga na hali zao zinaendelea vizuri.
Pia amesema kuwamtuhumiwa alikimbia mara baada ya tukio hilo na juhudi za
kumtafuta na kumkamata zinaendelea.
Aidha ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Shinyanga kuacha kabisa tabia ya
kujichukulia sheria mkononi na inapotokea kutoridhika na maamuzi ya mahakama
ni vyema kuchukua hatua ya kukata rufaa dhidi ya maamuzi ya mahakama badala
ya kujichukulia sheria mkononi mwao.