14.6 C
Nairobi
Thursday, August 5, 2021
Kenya
206,691
Total confirmed cases
Updated on August 5, 2021 6:33 am

SARAH OBAMA, BIBI YA RAIS WA ZAMANI BARACK OBAMA AFARIKI DUNIA

Sarah Obama, bibi ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amefariki dunia katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu akiwa na miaka...
More

  Latest Posts

  AWAONDOA WANAWE SHULENI AKIDAI ELIMU NI USHETANI

  Polisi mjini Nanyuki nchini Kenya,wanamzuilia mama mmoja mwenye umri wa miaka 36 ambaye aliwatoa wanawe shuleni akidai kwamba elimu ni ya kishetani.

  Mama huyo anayejulikana kama Esther Njeri, ni mama wa watoto wawili , binti wa miaka 13 na mvulana mwenye umri wa miaka 8.

  Kwa mujibu wa Chifu wa eneo hilo ambaye alipashwa habari na wazee wa eneo hilo, watoto hao wawili walikuwa hawajarudi shuleni tangu taasisi za elimu zilipofunguliwa Januari, 2021.

  Cha kushangaza ni kuwa Njeri amesoma na ana Shahada mbili, ya Biashara na nyingine ya Uhasibu. Majirani zake waliokuwa wamechangayikiwa walisema mama huyo alikuwa akiwaambia mwisho wa dunia unakaribia na hivyo aliishi kuwaonya kutubu kabla ya mwaka kukamilika. Alisema pia yuko tayari kukabiliana na sheria, akilinganisha masaibu yake na Shadrack, Meshack na Abednego wa Bibilia.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: