14.6 C
Nairobi
Thursday, August 5, 2021
Kenya
206,691
Total confirmed cases
Updated on August 5, 2021 7:33 am

SARAH OBAMA, BIBI YA RAIS WA ZAMANI BARACK OBAMA AFARIKI DUNIA

Sarah Obama, bibi ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amefariki dunia katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu akiwa na miaka...
More

  Latest Posts

  BASI LATUMBUKIA BAHARINI LIKONI

  Basi la watalii lilitumbukia Bahari Hindi nchini Kenya baada ya dereva kupoteza mwelekeo alipokuwa akiingia kwenye feri kuvuka upande wa pili kwenye kivuko cha Likoni jumapili Januari 10.

  Inaarifiwa basi hilo la kampuni ya Pollmans Tours and Safaris lilikuwa likitoka upande wa Pwani Kusini kuelekea Mombasa wakati kisa hicho kilifanyika Walioshuhudia kisa hicho wanasema dereva wa basi hilo alipoteza mwelekeo alipokuwa akijaribu kuingia kwenye feri. Ni dereva na utingo wake waliokuwa kwenye basi hilo na waliruka baharini kutoka kwenye basi na kujitosa baharini ambapo waliokolewa kwa mashuailyokuwa ikipiga doria baharini huku maafisa Shirika la Feri wakifaulu kulitoa basi hilo ambalo lilikuwa likiendelea kuzama.

  Ni Mwezi wa Disemba 2020 tu ambapo mkenya mwingine Winnie Achieng, alipoteza mwelekeo na kutumbukia kwenye bahari hiyo na kufariki dunia alipokuwa akikimbizwa hospitalini baada ya kuokolewa. Achieng’ alikuwa pamoja na mwanawe Gift Otieno wakati wa tukio hilo lakini mwanawe alifaulu kuogelea hadi nchi kavu.

  Kwa mujibu wa ripoti ya polisi zilisema kwamba ajali Ilifanyika wakati dereva alikuwa akijaribu kupita pikipiki iliyokuwa mbele yake lakini gari lake likagonga mawe na kupoteza mwelekeo na kutumbukia baharini.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: