Bawabu mmoja kutoka eneo la Sotik nchini Kenya awashangaza majirani kwa tabia yake ya kubeba godoro akienda kazini jioni na akitoka kazini asubuhi.
Inaarifiwa, jirani alikutana na bawabu huyo akiwa amebeba godoro akielekea kazini na akaamua kumuuliza sababu zake za kufanya hivyo kila jioni anapoondoka. Bawabu huyo alimjibu jirani kwamba mkewe sio mwaminifu na ndiposa anaamua kubeba godoro lake kwani hataki mkewe alalie na mchepuko wake au mpango wa kando wakifanya mapenzi wakati yeye yuko kazini. Hivyo hatua hiyo ilikuwa ni kumfunza mkewe adabu ili awache kutumia godoro lake kuzini wakati alitoa jasho kulinunua.
Inasemekana vicheko vilishamiri kwani hatua ya jamaa ilikuwa imevutia umati wa majirani waliokusanyika kujisikilia umbea. Duru zinaarifu kwamba mmoja wa majirani aliwanyamazisha na kuthibitisha madai ya jamaa kwamba kweli mama huyo alikuwa kiruka njia.