18.4 C
Nairobi
Saturday, May 8, 2021
Kenya
162,666
Total confirmed cases
Updated on May 8, 2021 10:17 am

GAVANA WA ZAMANI WA NAIROBI MIKE SONKO AACHILIWA KWA DHAMANA

Hatimaye aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko ameachiliwa kwa dhamana baada ya kuzuiliwa rumande kwa muda wa takribani mwezi mmoja. Kwa mujibu wa TUKONEWS, Sonko...
More

  Latest Posts

  BBI KUJADILIWA TENA NA WABUNGE JUMATANO NA ALHAMISI

  Wabunge wa bunge la Kenya wanatarajiwa kuwa na mkutano Jumatano 28 Aprili na Alhamisi 29 April mwaka mswada mkuu ukiwa ni mswada wa marekebisho ya Katiba Mwaka wa 2020 maarufu kama BBI.

  Wabunge wameishajulishwa na Spika wa Bunge la Kitaifa Justin Muturi kuhusu mikutano hiyo ikiwemo Mswada huo wa marekebisho ya Katiba ambao utajadiliwa kwa hatua zote; kusomwa kwa mara ya pili, kamati ya bunge nzima na kisha kusomwa kwa mara ya tatu.

  Hii ni baada ya kubainika kuwepo kwa mkanganyiko kuhusu aina mbili ya Miswada hiyo iliyowasilishwa katika Bunge la Kitaifa na lile la Seneti. Ikisemekana kuwa Seneti ndiyo ina Mswada sahihi wa BBI uliotoka katika Tume ya Uchaguzi, IEBC huku Bunge la Kitaifa likiwa na mswada tofauti kabisa.

  Mswada huo aidha utahitaji nusu ya wabunge watakaokuwa wamehudhuria kuunga mkono au kuupinga kabla ya kusomwa kwa mara ya pili na ya tatu.

  Baada ya mswada huo kupita bungeni kwa kura zinazohitaji ndipo sahihi za wananchi zitakusanywa tena.Hii ni kwa mujibu wa sharia za Kenya.

  Hata hiyvo Rais anatarajiwa kuiagiza Tume ya Uchaguzi, IEBC kuendesha kura ya maamuzi chini ya kipindi cha siku 90.
  Pia imebainika kuwa ni kaunti kumi na tatu tu zilizojadili na kuupitisha mswada sahihi ambazo ni Murang’a, Nakuru, Nyandarua, Nyeri, Embu, Tharaka Nithi miongoni mwa nyingine huku nyingine 34 zikiujadili mswada tofauti ambao mpaka sasa haijabainika ilikuwaje kukawa na katiba mbili tofauti.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: