Kizaazaa kilishuhudiwa kwenye soko la Mbui Nzau katika Kaunti ya Makueni kwenye barabara kuu ya Mombasa-Nairobi wiki hii nchini Kenya wakati gari moja lililokuwa likisafirisha mali ya Padre kuanguka huku wakazi wakiiba vifaa vya kufanya misa, mavazi ya Padre, divai pamoja na vifaa vya nyumbani vikiwamo vitanda na vifaa vya kielektroniki.
Aaron Ngolania ambaye pia ni kiongozi wa kanisa, alishuhudia kisa hicho na kuwahimiza wote walioiba bidhaa za Padre kuzirejesha.
Amewashukuru wote waliorejesha mali walioiba akisema si vyema kuiba mali ya mtu aliyehusika katika ajali bali wanafaa kumsaidia.