Bunge la Somalia limepiga kura ya kumwondoa kwenye wadhifa wake Waziri mkuu Hassan Ali Khayre, ambaye ameendelea kukosolewa kutokana na njia anavyoishughulikia hali ya usalama nchini humo.
Wabunge wamepiga kura ya kumvua uwaziri Hassan Ali Khayre kwa kura 170 na wabunge wanane wamepiga kura ya hapana, ametangaza spika wa bunge la Somalia.
Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed amesema katika taarifa kwamba anakubali uamuzi wa bunge kumvua uwaziri waziri mkuu wa nchi hiyo.