Cristiano Ronaldo Amfollow Mkenya Mmoja Tu Kule Instagram

0
167

Leo tupate kumjua mkenya pekee ambaye Cristiano Ronaldo mchezaji wa Juventus anamfuata au kumfollow kule instagram.Huyu ni mchezaji maarufu duniani lakini katika pitapita zangu kwenye mitandao ya kijamii hususan Instagram nimegundua kuwa Ronaldo kwenye official account yake amemfollow mkenya mmoja tu kati ya watu au accounts 449 anaowafollow.
Ronaldo ambaye ni mmoja wa wachezaji ambao wanafuatiliwa au wana followers wengi sana kwenye mitandao yao ya instagram,pia ndiye mchezaji wa kwanza kufikisha followers milioni 200 mwezi Januari mwaka huu.
Akitumia majina yake ya Cristiano Ronaldo hadi tukienda hewani yuko na followers milioni 220 na anawafollow watu au accounts 449.Pia nikiangalia facebook page yake ana likes milioni 122.Wow!
Sasa kulingana na kichwa chetu cha habari,Christiano Ronaldo anamfuatilia mkenya mmoja pekee kule instagram amabye si mwingine bali ni mkimbiaji maarufu Eliud Kipchoge,ambaye pia anamfollow Cristiano Ronaldo.

Our Sponsors

Leave a Reply