14.6 C
Nairobi
Thursday, August 5, 2021
Kenya
206,691
Total confirmed cases
Updated on August 5, 2021 6:33 am

SARAH OBAMA, BIBI YA RAIS WA ZAMANI BARACK OBAMA AFARIKI DUNIA

Sarah Obama, bibi ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amefariki dunia katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu akiwa na miaka...
More

  Latest Posts

  FAHAMU YATAKAYOFANYIKA KWENYE MAZIKO YA HAYATI MAGUFULI LEO

  Aliyekuwa Rais wa Tanzania,Magufuli aliyefariki dunia Machi 17, 2021 kwa ugonjwa wa moyo atazikwa katika kijiji cha Mlimani wilayani Chato nchini tanzania.

  Hivyo leo Ijumaa Machi 26,2021 ni huzuni na majonzi. Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anawaongoza viongozi mbalimbali wa Serikali ya Tanzania na nje ya nchi, majeshi ya ulinzi na usalama, vyama vya siasa, dini na wananchi katika mkoa wa Geita kwenye mazishi ya hayati John Magufuli.

  Kwa mujibu wa Sheria ya Maziko ya viongozi nchini Tanzania ya mwaka 2006 kifungu cha 20(1-4) inaeleza utaratibu siku ya mazishi ya Rais.

  Yafuatayo ni baadhi ya mambo ambayo yanatarajiwa kufanyika leo yakiwa katika mfumo wa taratibu za kijeshi nchini Tanzania.

  Kutakuwa na gwaride maalumu litakaloandaliwa na askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

  Wakati wa gwaride hilo litakaloandaliwa kwa heshima ya Rais anayezikwa, pia utaimbwa wimbo wa Taifa wa Tanzania.
  Pia askari wa JWTZ watapiga mizinga 21 wakati wa mazishi hayo karibu na eneo linalofanyika maziko ya Rais aliyefariki.

  Jambo lingine ni kwamba utaratibu mzima wa ufanyikaji wa gwaride hilo unatakiwa kufuata maelekezo ya Waziri ambaye ana dhamana ya kusimamia masuala ya ulinzi.

  Huku hayo yakiendelea,familia ya watu watano waliofariki jumapili Machi 21,2021 kwa kukanyagwa katikaUwanja wa Uhuru katika shughuli ya kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Tanzania,John Pombe Magufuli hatimaye walizikwa hapo jana huko Kimara jijini Dar es salam.

  Makaburi ya wanafamilia watano waliozikwa Machi 25,2021 jijini Dar es salaam

  Wanafamilia waliofariki dunia ni Susan Mtuwa na watoto wake wawili, Nathan (6) na Natalia (5) pamoja na watoto wengine wawili wa Shemeji zake ambao Michelle (8) na Christian (11) ambao ni watoto wa shemeji zake Susan pamoja na dada wa kazi wa familia hiyo aliyepatikana amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Mkoa wa Dar es Salaam.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: