Gavana wa kaunti ya Migori nchini Kenya Okoth Obado na wanawe wane watasalia korokoroni hadi Jumatatu Agosti 31 mwaka huu wakati mahakama itakapo amua iwapo wataachiliwa kwa dhamana au la.
Hakimu mkuu wa mahakama ya Milimani iliyoko Nairobi Lawrence Mugambi leo hii ametupilia mbali ombi lililowasilishwa na wakili wa Obado, Kioko Kilokumi la kutaka mteja wake aachiliwe akisubiri uamuzi huo.Mugambi amesema atatoa uamuzi huo Jumatatu wiki ijayo.
Mapema leo gavana obado na wanawe wane wamekana mashtaka ya ufisadi dhidi yao na kwamba walipanga kuiba shilingi 73.4M fedha za umma.Obado anatuhumiwa kuhusika na kampuni zilizopewa zabuni na serikali ya Kaunti ya Migori kisha pesa zikatumwa kwa akaunti za wanawe.Obado pia anamashtaka mengine manane kukiwemo utakatishaji wa fedha,mashtaka ambayo ameyakana.
Gavana huyo na mwanae Dan Okoth wameshtakiwa kwa Pamoja kwa kutumia shilingi 10 Milioni walizopata kinyume na sheria kununua gari aina ya Toyota Land Cruiser.Pia gavana huyo kulingana na shtaka ya Mkuu wa mashtaka ya Umma Noordin Haji pesa zingine zilitumika kuwalipia watoto wa Obado karo ya shule na mahitaji mengine. Mengi zaidi kuhusu mashtaka hayo — https://vuvu.co.ke/gavana-wa-migoriokoth-obado-na-wanawe-watatu-matatani/