Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma Noordin Haji ameagiza Gavana wa Kaunti ya Migori Zachary Okoth Obado na watoto wake watatu kuwa ni miongoni mwa watu 24 wanaostahili kukamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa madai ya wizi wa pesa za kaunti ya Migori nchini Kenya.
Katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari ,Haji amesema kuwa uchunguzi uliofanywa kati ya 2013,2014 na 2016,shilingi Milioni 73,474,356.90 zinadaiwa kuibwa kutoka kwa akaunti za kaunti hiyo ya Migori.Uchunguzi huo umebaini kuwa Obado na wanawe watatu Achola Dan Okoth,Susan Scarlet Okoth na Jerry Zachary Okoth waliiba kiasi kikubwa cha pesa kutoka kwa akaunti za Migori kwa kulipwa pesa kupitia kampuni mbalimbali.
Pesa za kaunti ya Migori kulingana na taarifa hiyo Haji zilitumiwa kuwalipia watoto wa Obado karo ya shule na matumizi mengine katika shule walizokuwa wakisomea nchini Australia, Scotland na Uingereza.
Kiasi cha shilingi Milioni 34,525,000 pia zilitumika kununua nyumba mtaani Loresho jijini Nairobi ambapo mmiliki ni mtoto wake Obado kwa jina Evelyne Adhiambo Zachary .Pia kiasi kingine cha pesa kilitumika kununua magari mawili ya kifahari ya aina ya Toyota Land Cruiser V8.
Hivyo taarifa hiyo inasema kuwa kuna ushahidi wa kutoshakumshataki obado na wanawe wote watatu kwa wizi wa pesa za Migori huku wanawe wakidaiwa kupewa pesa za wafanyikazi wa Kaunti ya hiyo.