14.6 C
Nairobi
Thursday, August 5, 2021
Kenya
206,691
Total confirmed cases
Updated on August 5, 2021 6:33 am

SARAH OBAMA, BIBI YA RAIS WA ZAMANI BARACK OBAMA AFARIKI DUNIA

Sarah Obama, bibi ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amefariki dunia katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu akiwa na miaka...
More

  Latest Posts

  GAVANA WA ZAMANI WA NAIROBI MIKE SONKO AACHILIWA KWA DHAMANA

  Hatimaye aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko ameachiliwa kwa dhamana baada ya kuzuiliwa rumande kwa muda wa takribani mwezi mmoja.

  Kwa mujibu wa TUKONEWS, Sonko aliachiliwa kwa dhamana ya KSh 500, 000 pesa taaslim Alhamisi, Machi 4.

  Mike Sonko akipelekwa Mahakama ya Kahawa

  ” Sonko ameachiliwa kwa dhamana lakini sina uhakika iwapo atakubaliwa kusafiri kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya kupokea matibabu spesheli kama ilvyopendekezwa na daktari wake,” Wakili wake alisema.

  Mike Sonko anatuhumiwa kuwafadhili magaidi, matumizi mabaya ya afisi na kupeana zabuni visivyo wakati alikuwa gavana. Hata hivyo Sonko alikana mashtaka au tuhuma hizo dhidi yake mbele ya Hakimu Mkuu wa Mahakama ya Kahawa Diana Mochache. Awali Hakimu Peter Ooko alikuwa ameelezewa kwamba Sonko hayuko kwenye hali nzuri ya kiakili kuwezi kujibu mashtaka dhidi yake.

  Kwa mujibu wa Wakili wa mwanasiasa huyo ni kwamba, Sonko alifanyiwa ukaguzi wa kiakili katika hospitali ya Aga Khan na ikabainika kwamba anaugua ugonjwa wa kiakili. Ingawa ripoti mbili za matibabu zimeonyesha kwamba Sonko ana matatizo ya kiakili.

  Hakimu Ooko alisema Mahakama itaamua iwapo mshukiwa yuko tayari kujibu mashtaka au la.

  Aidha, hakimu huyo ameamuru Sonko afanyiwe tena ukaguzi wa kimatibabu na mtaalamu wa magonjwa ya kiakili katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta.

  Ameachiliwa kwa dhamana siku moja tu baada ya kusherehekea siku ya kuzaliwa kwake,huku akitimiza miaka 46.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: