14.6 C
Nairobi
Thursday, August 5, 2021
Kenya
206,691
Total confirmed cases
Updated on August 5, 2021 7:33 am

SARAH OBAMA, BIBI YA RAIS WA ZAMANI BARACK OBAMA AFARIKI DUNIA

Sarah Obama, bibi ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amefariki dunia katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu akiwa na miaka...
More

  Latest Posts

  HIZI NDIZO ZAWADI RAIS UHURU KENYATTA AMEZITOA KWA WAKENYA LEO LEBA DEI

  Rais Uhuru Kenyatta katika hotuba yake ya kusherehekea leba Dei leo Mosi Mei, 2021 amepunguza masaa ya kafyu ya kutokuwa nje kuanzia saa mbili hadi saa nne usiku na itakamilika saa kumi asubuhi.

  Rais Uhuru Kenyatta ameondoa zuio la kuingia au kutoka na ameondoa masharti makali yaliyokuwa yamewekwa katika kaunti tano ambazo ni Nairobi,Kajiado,Machakos,Kiambu na Nakuru.

  Mikahawa na baa imeruhusiwa kufunguliwa hadi saa moja jioni.

  “Uuzaji wa pombe katika kaunti hizi utarejelewa ila hadi saa moja jioni. Na ninataka kurudia tena, hadi saa moja jioni pekee,” Rais Uhuru alisema.

  Aidha shughuli za ibada zitarejelewa kwa sharti kuwa waumini wawe ni theluthi moja pekee kwa kila kikao.

  Pia shughuli za michezo zimeruhusiwa kurejelewa .

  Zuio hilo la kutotoka na kuingia katika kaunti tano hizo nchini humu miongoni mwa masharti mengine,lilitangazwa na Rais Uhuru Kenyatta Machi 26,2021 na limetekelezwa takribani mwezi mmoja na siku chache ili kuzuia usambaaji wa virusi vya Corona.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: