Watu 599 wamethibitishwa kuambukizwa ugonjwa wa Covid19 nchini Kenya Hivyo jumla ya walioambukizwa ugonjwa huo nchini Kenya kufikia watu 26,436 katika masaa 24 yaliyopita kutoka jana waziri wa Afya alipoongea na wanahabari katika hotuba yake ya kila siku ya kuhusu Corona.Akiongea hivi leo akiwa kwenye Kaunti ya Kisumu,Waziri Wa Afya Mutahi Kagwe amesema sampuli zote zilizopimwa ni za watu 4,420 hivyo kufikia jumla ya sampuli 353,727 zilizopimwa tangu kutangazwa kwa uwepo wa Corona nchini Kenya.
Aidha kwa masaa 24 watu 1,062 wametangazwa kupona kutokana na ugonjwa huo hivyo kufikia 12,961 ya watu waliopona.Ikiwa ni idadi kubwa ya waliopona kuwahi kuripotiwa nchini Kenya.Watu 2 wameripotiwa kuaga dunia hivyo jumla ya walioiaga dunia kufikia 420.
Kaunti ya Nairobi imeripoti idadi kubwa ya walioambukizwa ugonjwa wa Covid19 ikiwa na 318,Kaunti ya Kiambu ikiwa na 70,Nakuru ikiwa na 39,Machakos 38,Machakos 38,Mombasa 28,Kajiado 26,Kericho 14,Isiolo 10,Kisii 9, Kakamega 6,Makueni 5,Kisumu 4,Kitui 4,Murangโa 4,Narok,Nyandarua,Nyeri na Kilifi zikiwa na idadi ya watu 3 kila kaunti.Meru na Busia zikiwa na watu 2 kila Kaunti .Siaya,Trans Nzoia,Wajir,Bomet,Garissa,Marsabit,Nandi na Nyamira zikiwa na idadi ya mgonjwa mmoja kila kaunti.