18.4 C
Nairobi
Saturday, May 8, 2021
Kenya
162,666
Total confirmed cases
Updated on May 8, 2021 10:17 am

GAVANA WA ZAMANI WA NAIROBI MIKE SONKO AACHILIWA KWA DHAMANA

Hatimaye aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko ameachiliwa kwa dhamana baada ya kuzuiliwa rumande kwa muda wa takribani mwezi mmoja. Kwa mujibu wa TUKONEWS, Sonko...
More

  Latest Posts

  JOE BIDEN AAPISHWA KUWA RAISI WA MAREKANI

  Joe Biden amekula kiapo na kuwa rais wa 46 wa taifa la Marekani. Biden alikula kiapo mbele ya jaji wa Mahakama Kuu John Roberts, January 20,2021.

  Baada ya kula kiapo Biden alilihutubia taifa kwa mara ya kwanza akiwa Rais wa Marekani.

  Mtangulizi wake, Donald Trump hakuhudhuria tukio hilo muhimu, na hatua hiyo imemfanya kuwa rais wa kwanza kutohudhuria sherehe za kuapa kwa mrithi wake tangu mwaka 1869.

  Pia Makamu wa Rais mteule Harris aliapishwa mbele ya Bwana Biden na kuwa mwanamke wa kwanza na mtu wa kwanza mweusi na mwenye asili ya Asia na Marekani aliyeinuliwa kuhudumu katika nafasi ya pili muhimu baada ya Urais.

  Shughuli za uapisho zilifanyika wakati kukiwa na ulizi mkali baada ya waandamanaji wanaomuunga mkono Trump kufanya vurugu tarehe 6 mwezi Januari.

  Sherehe hizo zilihudhuriwa na watu wachache kinyume na ilivyo desturi yake kwa sababu ya janga la corona.

  Joe Biden akiwa na umri wa miaka 78, ndiye rais wa Marekani mwenye umri mkubwa zaidi kuwahi kuapishwa.

  Sherehe hizo zilipambwa na watumbuizaji kama vile Lady Gaga,aliyeimba wimbo wa taifa, Jenifer Lopez na Garth Brooks.Akiwemo msichana mshairi Amanda Gorman mwenye umri Wa miaka 22.Baada ya kutumbuiza kwa shairi lake,Amanda amejizolea umaarufu zaidi kwenye mtandao Wa kijamii wa Instagram.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: