Bunge la Congres limemuidhinisha Joe Biden na Kamala Harris kama rais mteule na makamu wake wa Marekani.
Bunge hilo limewaidhinisha wawili hao kwa kura 282 huku wabunge 138 wakipiga kura ya kupinga matokeo ya jimbo la Pennsylvania.
Kura za wajumbe zilithibitishwa baada ya mabunge yote mawili lile la uwakilishi na lile la seneti kukataa pingamizi kuhusu kura zilizopigwa katika vituo vya jimbo la Pennsylvania na Arizona.
Shughuli za bunge zilikatizwa siku ya Jumatano wakati wafuasi wa Rais Trump walipovamia jumba la Capitol Hill na Bunge la Marekani ambapo katika vurugu hizo mtu mmoja (raia) alithibitishwa kufariki dunia baada ya kupigwa risasi huku maafisa wa polisi kadhaa kujeruhiwa.
Bunge la uwakilishi pamoja na lile la Seneti litaendelea kuhesabu kura za wajumbe zilizosalia ili kumuidhinisha Joe Biden kuwa rais mtarajiwa wa Marekani.