Wanakijiji wa Luanda katika Kaunti ya Vihiga nchini Kenya wamepatwa na mshangao baada ya kuku kukataa kuuzwa sokoni.
Kwa mujibu wa mmoja wa wanakijiji hao ambaye alishuhudia tukio hilo,ni kwamba jogoo huyo anadaiwa kuibwa na mwanaume mmoja kwa jina William, kutoka katika kaunti ya Siaya alikataa kuuzwa hata baada ya wanunuaji kupatikana licha ya kunadiwa kwa bei nafuu.Amesema kila alipopatikana mtu Wa kumnunua jogoo huyo alikatalia mikononi mwa William.
Tukio hilo lilitokea na kujirudia mara 4 hadi watu waliokuwa sokoni walianza kushuku na kuamua kumkabili mtu huyo. Walimhoji kumhusu jogoo huyo ambaye bei yake ilikuwa KSh 800 ambayo kwa kawaida ni shilingi 1200 na zaidi.
Wafanyabiashara katika soko hilo, walimhoji William na kutaka kufahamu ni kwa nini jogoo huyo alikuwa akionyesha tabia isiyokuwa ya kawaida.
Kwa kuwa soko hilo lipo mpakani, inadaiwa mwenye kuku huyo alikuwa katika soko hilo baada ya kupata taarifa ya tukio la sokoni alifika na kumtambua kuku huyo kuwa wake aliyekuwa ametoweka.
Katika hali ya kushangaza sana, mtu huyo alisema amefanya urafiki mkubwa na mifugo wake, na kwamba ni vigumu mtu yeyote kumwibia.
Aliondoka na kuku wake huku William akiponea kichapo kutoka kwa wanakijiji hao.