Kadinali wa kanisa Katoliki John Njue amejiuzulu rasmi ukadinali baada ya kuhitimu umri wa kustaafu.
Taarifa za kujiuzulu kwa Njue zimetolewa rasmi Roma leo Jumatatu Januari 4 huku ikiibuka pia kustaafu kwa maaskofu kanisani Katoliki hujulikana kama kujiuzulu kulingana na sheria za Kanisa la Katoliki. Kulingana na sheria hizo, askofu akihitimu miaka 75 humwandikia Kiongozi wa Kanisa hilo, Papa barua ya kujiuzulu na kisha kusubiri uamuzi wa Papa.
Njue atakumbukwa kwa kuwa na msimamo mkali kwenye suala la ndoa za jinsia moja.Kadinali Njue amekuwa Askofu Mkuu wa dayosisi ya kanisa Katoliki Nairobi tangu mwaka wa 2007 na uamuzi wake wa kujiuzulu umekubaliwa na Papa Francis ambaye ni kiongozi wa kanisa hilo.
“Ukristo wetu uko wapi wakati ambapo tunaruhusu mwanaume kuoa mwenzake au mwanamke kwa mwanamke mwenzake? Ukikula uchafu pia wewe utakuwa mchafu, kwendeni huko na hiyo tabia mbaya,” alisema Njue 2015. Aidha,Suala hilo la ndoa za jinsia moja kanisani humo lilichukua mkondo mpya baada ya uongozi wa Roma kuziunga mkono.
Kwa sasa Kadinali mpya David Kamau ameteuliwa na Papa kuwa msimamizi wa dayosisi ya Nairobi.