KASISI MKAIDI

0
137

Kasisi wa kanisa moja kule Kitui aliyepona kutokana na virusi vya acorona baada ya kurejea nchini Kenya kutoka mjini Roma  nchini Italia,ameandikisha taarifa katika kituo cha polisi cha Kitui.

Hii ni siku moja tu baada ya kuachiliwa kutoka hospitali ya wagonjwa ya corona waliotengwa ya Mbagathi jijini Nairobi alikokuwa akipokea matibabu.

Kasisi Nicholus Maanzo wa kanisa katoliki alirejea nchini tarehe 23 mwezi wa 3 mwaka huu kutoka Italia na kudaiwa kukaidi agizo la kujitenga kwa siku 14.Hii iliwalazimu maafisa wa polisi wa kitui kumtenga kwa lazima nyumbnani kwake katika kijiji cha Misewani-Kitui ya Kati.Ambapo baadaye alipatikana kuwa na virusi vya corona na kupelkwa kituo cha Mbagathi jijini Nairobi.

Kasisi Maanzo aliye na umri wa miaka 60, alitibiwa na kuruhusiwa kurejea nyumbani hapo jana.

Kwa sasa anatakiwa kuelekea katika kituo hiccho cha polisi ijumaa wiki ijayo/hii ili kufikishwa katika mahakama ya Kitui kujibu mashtaka.

Our Sponsors

Leave a Reply