14.6 C
Nairobi
Thursday, August 5, 2021
Kenya
206,691
Total confirmed cases
Updated on August 5, 2021 7:33 am

SARAH OBAMA, BIBI YA RAIS WA ZAMANI BARACK OBAMA AFARIKI DUNIA

Sarah Obama, bibi ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amefariki dunia katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu akiwa na miaka...
More

  Latest Posts

  KIFO CHA MAGUFULI: SIKU 7 ZA MAOMBOLEZO KENYA NA 14 TANZANIA

  Rais Uhuru Kenyatta ametangaza siku saba za maombolezo nchini Kenya kufuatia kifo cha Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania na bendera zitapepea nusu mlingoti.
  Pia Rais Uhuru ametoa pole kwa Watanzania wote kwa ujumla na kwa Mama Janeth ambaye ndiye mama Taifa na mke wa Rais Magufuli.

  “Nimempoteza Rafiki, nimempoteza Kiongozi mwenzangu na Kenya tunasimama imara na wenzetu Watanzania kwenye wakati huu mgumu, nimeongea na Mama Samia nimempa pole na kumuhakikishia tunasimama nae pamoja kwenye wakati huu mgumu” Ujumbe wa Rais Uhuru Kenyatta.

  Vilevile nchi ya Tnzania itakuwa na maombolezo ya Siku 14 na bendera zitapepea nusu mlingoti.Hii ni kwa mujibu wa Makamu wa Rais wa Tanzania Mama Samia Suluhu aliyetangaza habari za kifo cha Rais Magufuli hapo jana Machi 17,2021.

  “Rais Magufuli amefariki kwa maradhi ya moyo katika Hospitali ya Mzena, alilazwa March 6 2021 katika Hospitali ya Jakaya Kikwete na kuruhusiwa March 7 na kuendelea na majukumu yake”

  “March 14 alijisikia vibaya na akarudi Hospitali ya Mzena ambapo aliendelea na matibabu hadi umauti unamkuta, Nchi yetu itakuwa na maombolezo ya siku 14 na bendera zitapepea nusu mlingoti.’’ alisema Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu.

  Aidha, mipango ya mazishi ya Rais huyo itatangazwa baadae na Serikali ya Jamhuri ya Tanzania.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: