14.6 C
Nairobi
Thursday, August 5, 2021
Kenya
206,691
Total confirmed cases
Updated on August 5, 2021 6:33 am

SARAH OBAMA, BIBI YA RAIS WA ZAMANI BARACK OBAMA AFARIKI DUNIA

Sarah Obama, bibi ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amefariki dunia katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu akiwa na miaka...
More

  Latest Posts

  KIJANA ATOKWA UTUMBO SEHEMU YA HAJA KUBWA BAADA YA KUIBA PES

  Kijana mmoja amejikuta pabaya baada ya kuiba pesa za mamalishe anayefahamika kwa jina la Catherin Peter mkazi wa Mtaa wa Kagongwa wilayani Kahama mkoani Shinyanga nchini Tanzania, tukio hilo limetajwa kuhusishwa na imani za Ushirikina,mnamo January 17,2021.

  Kutokana na kusambaa kwa video katika mitandao ya kijamii ikimuonesha kijana mmoja ambaye hajafahamika jina wala makazi akiwa amechuchumaa huku utumbo ukiwa umetoka katika sehemu zake za haja kubwa, muda mfupi baada ya kutuhumiwa kuiba pesa Bi. Catherin.

  Mwenyekiti wa Mtaa huo, Michel Shija akizungumza na mwanahabari wa Malunde Blog amekiri kutokea kwa tukio hilo Jumapili Januari 17,2021 majira ya saa 4 asubuhi ambapo inadaiwa mwizi huyo ambaye mpaka sasa hajafahamika jina wala makazi alifika katika mgahawa wa Catherin na kuomba kupatiwa maji ya kunywa mara baada ya kumaliza aliiba pesa shilingi elfu 90 zilizokuwepo kwenye mkoba ndipo aliulizwa akatupa zingine chini na kuanza kukimbia huku akikimbia na shilingi elfu 27 mkononi.

  Amefafanua kuwa mwizi huyo alikimbizwa na vijana waliokuwa karibu na eneo la tukio,baada ya kukimbia umbali mrefu ndipo akanguka chini na kuanza kuvua nguo zake huku utumbo ukiwa umening’inia kwenye sehemu za haja kubwa za mwili wake.Kitendo ambacho kiliwaogopesha watu wote walikuwa wanamkimbiza na kulazimika kumpeleka kituo cha polisi Kagongwa kwa taratibu za kisheria zaidi.

  Mwanaseni Ndullu mamalishe shuhuda wa tukio hilo amesema kuwa tukio hilo limezua taharuki kubwa kwa wakazi wa mtaa huo kwani haijawahi kutokea hata siku mmoja,mtu kupata madhara kama alivyopata mwizi huyo na kuwataka vijana kufanya kazi halali na kuachana na vitendo vya uhalifu mdogo mdogo.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: