14.6 C
Nairobi
Thursday, August 5, 2021
Kenya
206,691
Total confirmed cases
Updated on August 5, 2021 8:34 am

SARAH OBAMA, BIBI YA RAIS WA ZAMANI BARACK OBAMA AFARIKI DUNIA

Sarah Obama, bibi ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amefariki dunia katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu akiwa na miaka...
More

  Latest Posts

  KIJIJI CHA AJABU ZAIDI DUNIANI

  Kijiji cha Mafi Dove kilichopo kusini mwa nchi ya Ghana, chenye wakazi takribani 5000, lakini
  hakuna kati yao aliyezaliwa kijijini hapo kutokana na mila inayokataza watoto kuzaliwa.

  Kama ilivyo kwa vijiji vingi kuwa na tamaduni zao, kijiji cha Mafi Dove kimekuwa na mila hii
  ambayo imegeuka kuwa mwiba kwa wanawake, kwani wanapokuwa wajawazito na kutaka
  kujifungua, hulazimika kuondoka kijijini hapo na kwenda kijiji cha jirani, ili aweze kujifungua
  mtoto wake na kisha kurudi.
  Kuna Sauti ilitoka mbinguni na kuwajia mababu wa hicho kijiji enzi hizo, sauti kutoka mbinguni
  ilisikika ikiwaambia kuwa kijiji hicho ni mahali patakatifu, hivyo ukitaka kuishi hapo ni lazima
  ufuate masharti, sheria ya hapa ni,hakuna mtu anayeruhusiwa kuzalia hapa.
  Hiyo ni moja tu ya mila za ajabu zinazopatikana kijijini hapo, kwani zipo mila zingine ambazo pia
  wakazi wake wanazitekeleza mpaka sasa, ikiwepo kutofuga mnyama yeyote au hata ndege wa
  kufuga, na pia hawaruhusiwi kuchinja mnyama yeyote.
  Lingine la kushangaza zaidi katika kijiji hicho ni kwamba hakina kaburi hata moja, kwani pia
  hawaruhusiwi kuzika wafu, hivyo mtu akifa hulazimika kwenda nje ya kijiji ili kuzika ndugu yake.
  Mpaka sasa mila hizo zinaendelea kutekelezwa, huku baadhi ya wanawake wakilalamika kupata
  shida kubwa kwa sababu ya mila ya kutojifungua kijijini hapo, kwani hulazimika kutembea
  umbali mrefu kwenda kijiji kingine kujifungua.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: