16.1 C
Nairobi
Sunday, September 26, 2021
Kenya
248,392
Total confirmed cases
Updated on September 26, 2021 9:40 am

SARAH OBAMA, BIBI YA RAIS WA ZAMANI BARACK OBAMA AFARIKI DUNIA

Sarah Obama, bibi ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amefariki dunia katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu akiwa na miaka...
More

  Latest Posts

  KIKONGWE WA MIAKA 82 AKATWA MGUU WA KULIA BADALA YA KUSHOTO

  Mzee mgonjwa mwenye umri wa miaka 82 amekatwa mguu wake wa kulia badala ya kushoto katika hospitali moja ilioko wilaya ya Freistadt ya Austria.

  Imeripotiwa kuwa mgonjwa huyo ambaye ana maradhi yaliyoathiri miguu yake miwili, alitakiwa kufanyiwa upasuaji na kukatwa mguu wake wa kushoto kwani mguu wake wa kulia ulikuwa bado ni mzima.

  Kama ilivyo ada,kabla ya wagonjwa wa kufanyiwa upasuaji, huwekwa alama sehemu za mwili zinazofaa kufanyiwa upasuaji.Hivyo,Madaktari wa hospitali hiyo walifanya makosa kabla ya upasuaji na kuweka alama kwenye mguu wake wa kulia badala ya kushoto kwa ajili ya kukatwa.

  Hospitali hiyo imekiri kutokea kwa kosa hilo na imeeleza kuwa mgonjwa huyo anapewa msaada wa kisaikolojia huku uchunguzi zaidi wa tukio hilo ukiendelea ili kuzuia jambo kama hilo kutokea tena.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: