14.6 C
Nairobi
Thursday, August 5, 2021
Kenya
206,691
Total confirmed cases
Updated on August 5, 2021 8:34 am

SARAH OBAMA, BIBI YA RAIS WA ZAMANI BARACK OBAMA AFARIKI DUNIA

Sarah Obama, bibi ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amefariki dunia katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu akiwa na miaka...
More

  Latest Posts

  KISII: KAMANDA WA POLISI APATIKANA AMEAGA DUNIA NDANI YA GARI LAKE

  Kamanda huyo kwa jina Simon Gababa alimpigia simu dereva wake CPL wa polisi Abel Ondora akimtaka aje ampeleke hospitalini kwani hangeweza kujiendesha.

  Dereva aliwasili nyumbani kwa Gababa na kumkuta bosi wake amepoteza fahamu ndani ya gari lake la kibinafsi lililokuwa limeegeshwa nje ya makaazi ya wafanyikazi karibu na Taasisi ya Teknologia ya Ujenzi wa Barabara iliyoko Milimani,Kisii Mjini.

  Afisa huyo ambaye ni kamanda wa kituo cha polisi cha Kisii Central Simon Gababa aliaga dunia Jumamosi(leo) ,asubuhi.

  Taarifa iliyoandikishwa katika kituo hicho cha polisi ilionesha Gababa alimpigia simu dereva wake akimtaka aje ampeleke hospitalini kwani yeye mwenyewe hangeweza kujiendesha.

  Akithibitisha kisa hicho, kamanda wa polisi wa kaunti hiyo Jebel Munene alisema Gababa alikuwa ameugua kwa muda.

  “Amekuwa akimeza dawa kwa muda na alitazamia kupata nafuu. Ni siku ya huzuni kwa maafisa wa polisi hapa Kisii kufuatia kisa hicho,” alisema.

  Mwili wake ulipelekwa katika makafani ya hospitali ya rufaa ya mafunzo ya utabibu Kisii kusubiri upasuaji.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: