Idadi ya watu walioaga dunia kutokana na mafuriko na maporomoko ya ardhi katika kaunti ya Pokot
Magharibi nchini Kenya yalitokea usiku imefikia kumi na mbili.Hii ni baada ya miili saba kupatikana leo
kutoka kwa vifusi vya maporomoko hayo katika eneo la Chesogon ambako kulitokea mkasa huo.Huku
afisa mmoja wa polisi kuaga dunia wakati akipokea matibabu katika hospitali ya rufaa ya MTRH huko
Eldoret kutokana na majeraha aliyoyapata .
Mshirikishi wa serikali huko Bonde La Ufa,Bw. George Natembeya, ameyaweka hayo wazi.
Mvua kubwa inayoshuhudiwa kwa sasa nchini Kenya itaendelea kwa muda .Hii ni kwa mujibu wa Idara
ya Utabiri wa hali ya hewa.Na huenda kukawa na mafuriko zaidi katika baadhi ya maeneo.