14.6 C
Nairobi
Thursday, August 5, 2021
Kenya
206,691
Total confirmed cases
Updated on August 5, 2021 7:33 am

SARAH OBAMA, BIBI YA RAIS WA ZAMANI BARACK OBAMA AFARIKI DUNIA

Sarah Obama, bibi ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amefariki dunia katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu akiwa na miaka...
More

  Latest Posts

  MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA CORONA YAFIKIA 3.5 DUNIANI


  Maambukizi ya virusi vya Corona duniani yamefikia milioni 3.5 leo Jumatatu, wakati idadi ya vifo vinavyosababishwa na janga hilo imeongezeka hadi zaidi ya 245,000, ingawa viwango vya maambukizi mapya na vifo vimepungua ikilinganishwa na mwezi uliopita, kulingana na ripoti ya shirika la habari la Reuters.

  Visa vingi vilivyothibitishwa katika siku za hivi karibuni viliripotiwa katika ukanda wa Marekani ya Kaskazini na nchi za Ulaya, ingawa idadi ya kila siku ya maambukizi mapya inaongezeka katika ukanda wa Marekani ya Kusini, Afrika na Urusi.

  Duniani kote, visa vipya 84,004 viligunduliwa ndani ya masaa 24 yaliyopita, shirika la habari la Reuters limebaini, huku likijikita katika takwimu rasmi zilizotolewa na kila, idadi ambayo inafanya jumla ya visa duniani kote kufikia zaidi ya milioni 3.5.

  Vifo vinavyotokana na mlipuko wa Covid-19, ugonjwa unaosababisha matatizo ya kupumua vimefikia jumla ya 245,992.

  Huku Kenya ikithibitisha maambukizi mapya 25 ya virusi vya Corona na kufikisha 490 waliothibitishwa kuwa na virusi hivyo kufikia sasa.

  Wizara ya afya inasema kuwa visa 15 vinatoka jijini Nairobi na 10 kutoka kaunti ya Mombasa.

  Wote wakiwa ni wakenya ambao hawana historia ya kusafiri nje ya nchi.

  Naibu waziri wa afya Dkt Mercy Mwangangi anasema kuwa sampuli 1012 zilifanyiwa vipimo katika muda wa saa 24 zilizopita.

  Aidha watu 6 zaidi wamepona na kuruhusiwa kuondoka hospitalini na kufikisha 173 waliopona kufikia sasa.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: