14.6 C
Nairobi
Thursday, August 5, 2021
Kenya
206,691
Total confirmed cases
Updated on August 5, 2021 7:33 am

SARAH OBAMA, BIBI YA RAIS WA ZAMANI BARACK OBAMA AFARIKI DUNIA

Sarah Obama, bibi ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amefariki dunia katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu akiwa na miaka...
More

  Latest Posts

  MAMA NA WATOTO WAKE WAFUNGIWA NDANI YA NYUMBA KWA KUSHINDWA KULIPA KODI

  Polisi kule Njoro kaunti ya Nakuru nchini Kenya wanamsaka mhudumu mmoja wa nyumba za kukodi eneo la Egerton baada ya kumfungia ndani ya nyumba mpangaji mmoja tangu saa kumi na moja jana jioni baada ya kushindwa kulipa kodi ya nyumba ya shilingi 10000.
  Rhoda Phoebe Makhoha mama wa watoto watano ,amesema kuwa ameishi kwenye nyumba hiyo kama mpangaji kwa miaka 6 sasa na kwamba hakuweza kupata pesa za kulipa kodi kutokana na athari ya janga la Ugonjwa wa corona katika biashara yake ya kibanda tangu ugonjwa huo uzuke Kenya miezi minne iliyopita.
  Phoebe amesema kuwa alijaribu kumsihi msimamizi wa nyumba hiyo asimfungie lakini rai zake ziliambulia patupu na akafungiwa ndani ya nyumba hiyo kwa kuuchomelea mlango kwa chuma hapo jana.
  OCPD wa Njoro Mohamed Huka, aliitikia kilio cha wananchi wa eneo hilo na kumjuza OCS wa Njoro ambaye pamoja na maafisa wengine wa polisi waliingia ndani ya nyumba hiyo kwa kuuvunja mlango na kumuokoa mama huyo mwenye umri wa makamo pamoja na mwanae wa mwaka mmoja unusu ambaye anaugua.
  OCPD wa Njoro amewaonya vikali wamiliki wa nyumba za upangaji na wasimamizi dhidi ya kujihusisha na vitendo vya aina hiyo,akisema kuwa huyu msimamizi atatumika kama mfano wa wamiliki wengine wa nyumba waliyo na tabia ya kuwahangaisha wapangaji wao.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: