14.6 C
Nairobi
Thursday, August 5, 2021
Kenya
206,691
Total confirmed cases
Updated on August 5, 2021 8:34 am

SARAH OBAMA, BIBI YA RAIS WA ZAMANI BARACK OBAMA AFARIKI DUNIA

Sarah Obama, bibi ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amefariki dunia katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu akiwa na miaka...
More

  Latest Posts

  MAMA SAMIA SULUHU HASSAN NDIYE RAIS MPYA TANZANIA

  Leo Ijumaa Machi 19, 2021, Samia Suluhu Hassan ameapishwa kuwa Rais wa sita wa Tanzania. Ameapisha na Jaji Mkuu Ibrahim Juma katika Ikulu ya Tanzania jijini Dar es salam.
  Mama Samia ameapishwa katika hafla ndogo iliyofanyika katika Ikulu ya Magogoni na kuhudhuriwa na marais wastaafu wa Tanzania na Zanzibar.

  Mara baada ya kuapishwa alipigiwa mizinga ishirini na moja na kukagua gwaride maalumu kwa mara ya kwanza akiwa kama amiri jeshi mkuu wa majeshi ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.

  Rais Samia Suluhu akihutubia watu mara baada ya uapisho wake

  Mama Samia mwenye miaka 61 na mama wa watoto wanne,ameweka historia ya kuwa rais wa kwanza Mwanamke nchini Tanzania na wa pili Afrika Mashariki baada ya Slyvie Kiningi aliyeshika nyadhifa ya urais nchini Burundi.

  Mama Samia amechukua nafasi hiyo ya aliyekuwa rais wa Tanzania,  John Pombe Joseph Magufuli aliyefariki dunia Machi 17, 2021 kwa maradhi ya moyo katika hospitali ya Mzena alikokuwa akipatiwa matibabu.
  Hafla hiyo imafanyika kwa kufuata Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania inayonukuliwa hapa, Katika ‘’ Ibara ya 37 (5) Endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Rais kufariki dunia, kujiuzulu, kupoteza sifa za uchaguzi au kutomudu kazi zake kutokana na maradhi ya mwili au kushindwa kutekeleza kazi na shughuli za Rais, basi Makamu wa Rais ataapishwa na atakuwa Rais kwa muda uliobaki katika kipindi cha miaka mitano na kwa masharti yaliyoelezwa katika ibara ya 40, kisha baada ya kushauriana na chama cha siasa anachotoka Rais atapendekeza jina la mtu atakayekuwa Makamu wa Rais na uteuzi huo utathibitishwa na Bunge kwa kura zisizopungua asilimia hamsini ya Wabunge wote.’’

  Rais Samia atashikilia wadhifa huo kwa kipindi kilichosalia cha muhula wa urais mpaka 2025, kwa mujibu wa katiba ya Tanzania.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: