14.6 C
Nairobi
Thursday, August 5, 2021
Kenya
206,691
Total confirmed cases
Updated on August 5, 2021 7:33 am

SARAH OBAMA, BIBI YA RAIS WA ZAMANI BARACK OBAMA AFARIKI DUNIA

Sarah Obama, bibi ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amefariki dunia katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu akiwa na miaka...
More

  Latest Posts

  MAOMBI YA PASTA NA MKEWE KWA MLEVI YAWATIA MATATANI

  Mwanaume mmoja kutoka Mwingi, Kitui nchini Kenya aliyekuwa na mazoea ya kulewa na kuhangaisha kijiji kwa matusi alimfurusha mchungaji na mke wake waliokuwa wameenda kumuombea atokwe na pepo wa ulevi ili kubadilika.

  Kwa mujibu wa Taifa Leo, mwanaume huyo ambaye jina lake limehifadhiwa alipandwa na mori alipowaona na kuanza kuwafokea na kuwatishia akiwa amejihami kwa rungu na mjeledi. Pasta na mkewe hawakuwa na budi ila kukimbia ili kujinusuru kutoka kwa hatari iliyokuwa imewakodolea macho.

  “Mkithubutu kurejea hapa kwangu rungu langu litafanya kazi. Nikitaka kusikia neno la Mungu nitawatafuta kanisani,” mwanaume huyo alisikika akiwafokea.

  Kulingana na wanakijiji, walikuwa wamepeleka malalamiko yao kwa chifu wa eneo hilo na mwanaume huyo akaonywa kuhusu tabia yake na siku hiyo alilewa hata zaidi na akadhubutu kumtusi chifu mwenyewe. Alizuiliwa katika seli kwa siku kadhaa na kisha kuachiliwa baada ya kuuza pikipiki yake na kulipa faini yake.Lakini haku badilika. siku hiyo alilewa hata zaidi na akadhubutu kumtusi chifu mwenyewe.

  Hivyo wanakijiji hao wakaamua kumwendea pasta kulalamika kuhusu tabia ya mwanaume huyo ambaye walisema alikuwa akiwahangaisha wakati akiwa mlevi. Kulingana nao, mwanaume huyo alikuwa mtu muungwana na mpole wakati hajaonja pombe lakini punde tu alipopata na kunywa kileo chake alidhihirisha ushetani mwingi uliokuwa moyoni wake. Alipenda kuwakejeli wenyeji na kuwatusi hasa wale aliohisi walikuwa adui zake.

  Hata hivyo, wanakijiji wanaamini kwamba mui huwa mwema na kwamba siku moja hivi karibuni mwanaume huyo ataacha ulevi na kuwahangaisha wanakijiji.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: