Miezi kadhaa baada ya virusi vya corona kuingia nchini Kenya.Kungali kuna maswali chungu nzima kuhusiana na usahihi wa matokeo yanayotolewa na maabara kuhusu virusi vya covid 19.Haya yameibuka baada ya maabara moja nchini Kenya kutoa matokeo yasiyo sahihi yakiashiria kwamba mgonjwa mmoja alifariki kutokana na virusi vya Corona.
Wizara ya afya imesema kuwa inachunguza swala hilo na hatua itachukuliwa kwa maabara yoyote itakayopatikana kuwa na utepetevu kazini.
Hayo yanajiri huku Kenya ikirekodi visa vingine 307 zaidi na kufikisha 6673 jumla ya idadi ya watu walio na virusi vya corona nchini. Idadi hii ikiwa ni idadi ya juu zaidi kuwahi kurekodiwa Kenya tangu virusi vya corona kutangazwa kuingia nchini zaidi ya miezi 3 iliyopita.