16.1 C
Nairobi
Sunday, September 26, 2021
Kenya
248,392
Total confirmed cases
Updated on September 26, 2021 8:39 am

SARAH OBAMA, BIBI YA RAIS WA ZAMANI BARACK OBAMA AFARIKI DUNIA

Sarah Obama, bibi ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amefariki dunia katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu akiwa na miaka...
More

  Latest Posts

  MAWAZIRI 10 KATI YA 11 SUDAN KUSINI WAAMBUKIZWA CORONA

  Mawaziri 10 wameambukizwa virusi vya corona, hili limethibitishwa na msemaji wa serikali ya Sudan Kusini.

   

  Waziri wa Habari wa Sudan Kusini Michael Makuei ameiambia BBC kuwa mawaziri wote hao walikuwa ni wajumbe wa kamati ya juu ya serikali ya kupambana na virusi vya corona nchini humo na kuwa mawaziri hao wamepata maambukizo baada ya kukutana na aliyekuwa mjumbe wa kamati hiyo ambaye alikuwa na virusi vya corona.

   

  Katika mawaziri waliopo kwenye kamati hiyo, ni Waziri wa Afya pekee ambaye hajakutwa na maambukizi.Mawaziri wote 10 wamejitenga kwa sasa na serikali imesema kuwa wote wanaendelea vizuri kiafya.

   

  Taarifa za kuambukizwa kwa mawaziri hao zinakuja siku chache baada ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa nchi hiyo Riek Machar kutangaza kuwa amekutwa na virusi pamoja na mkewe, ambaye ni Waziri wa Ulinzi.

   

  Aidha Walinzi wa viongozi kadhaa nchini humo wamekutwa na virusi na kwa sasa wapo karantini.

   

  Mpaka sasa zaidi ya watu 300 wamethibitishwa kupata corona Sudan Kusini, huku watu wane wakipona na sita kufariki.

   

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: