Januari 12, 2021 nchi ya Malawi ilipata pigo baada ya mawaziri wawili kufariki dunia kutokana na Covid-19.
. Waziri Lingson Belekanyama
Waziri wa Habari wa Malawi, Gospel Kazako, amethibitisha kuwa mawaziri hao ambao ni Waziri wa Serikali za Mitaa, Lingson Belekanyama na Waziri wa Uchukuzi, Sidik Mia, wamefariki ndani ya masaa mbili.
Waziri Sidik
Mwishoni mwa juma lililopita, Rais wa nchi hiyo, Lazarus Chakwera, kupitia kwa njia ya radio alitoa hotuba kwa taifa na akatoa wito wa kuheshimiwa kwa hatua zilizowekwa za kupambana na maambukizi ya Covid-19 kufuatia ongezeko kubwa la maambukizi ya virusi hivyo na katika vifo.
Mnamo leo Januari 13, Rais Chakwera ametangaza hali ya dharura kukabili janga la Corona kwa wilaya zote 28 nchini humo baada ya vifo vya zaidi ya watu 50 wakiwemo mawaziri hao na maambukizi ya zaidi ya watu 2000 yaliyoripotiwa kutoka Januari 1,2021.