Mbunge wa Juja nchini Kenya, Francis Munyua Waititu amefariki dunia.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa familia yake ambayo ilithibitisha kifo chake, Waititu maarufu kama
Wakapee aligundua kuwa ana Saratani mwaka wa 2017, baada ya dada yake Cecilia Wambui, mwenye umri wa miaka 60 kuaga dunia mwaka 2016 kutokana na Saratani,kisha Mbunge huyo akaamua kumpeleka mamake mzazi kupimwa saratani.Kitu ambacho familia haikutegemea ,mamake aligundulika kuwa ana Saratani ya Ubongo.Kisha Mbunge huyo ambaye hakuwa anaumwa na popote wala kuonyesha dalili zozote za kuumwa, akachukua hatua ya kupima pia na akagundulika kuwa vilevile ana Saratani ya Ubongo mnamo Septemba 2017.Tangu hapo alienda kwa matibabu zaidi nchini India kwa muda wa wiki saba,kisha akarudi nchini Kenya machi 2018.
Na Disemba 2020 ziliibuka ripoti kuwa, mbunge huyo alikuwa hajifahamu tena.
Ameacha watoto wane na mke.