14.6 C
Nairobi
Thursday, August 5, 2021
Kenya
206,691
Total confirmed cases
Updated on August 5, 2021 8:34 am

SARAH OBAMA, BIBI YA RAIS WA ZAMANI BARACK OBAMA AFARIKI DUNIA

Sarah Obama, bibi ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amefariki dunia katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu akiwa na miaka...
More

  Latest Posts

  MBUNGE WA KIAMBAA PAUL KOINANGE AFARIKI DUNIA

  Mbunge wa Kiambaa Paul Koinange ameaga dunia.

  Maafisa katika Bunge na familia ya mbunge huyo wamethibitisha kuwa Mbunge huyo alifariki leo asubuhi Machi 31,2021 kutokana na maradhi ya Covid-19 alipokuwa akipokea matibabu katika Hospitali ya Nairobi.
  Hadi kufariki kwake Koinange alikuwa akihudumu kama mbunge wa Kiambaa kuanzia mwaka 2017 alipochaguliwa kupitia kwa chama Tawala cha Jubilee na pia alikuwa mwenyekiti wa kamati ya bunge ya utawala na usalama wa kitaifa.

  Kufuatia kifo cha mbunge huyo, Rais Uhuru Kenyatta aliongoza viongozi wengine nchini kutuma risala za rambi kwa familia ya mbunge huyo na wananchi wa Kiambaa.

  Katika ujumbe wake Rais Kenyatta alisema kwamba amempoteza kiongozi thabiti  ambaye lengo lake limekuwa kuunganisha wakenya  na kuendeleza taifa.

   “Kupitia Kamati ya Bunge ya Utawala na Usalama wa Kitaifa ambapo alikuwa Mwenyekiti, Mhe Koinange aliendeleza sheria na hatua za sera ambazo zilitaka kuunda taifa lenye amani na utulivu,” Uhuru alisema. 

  Kifo chake kinajiri siku chache tu baada ya taarifa kuenea kwenye mitandao ya kijamii kwamba kuna wafanyakazi wa bunge wengine wamelazwa katika hospitali mbalimbali humu nchini wakisumbuliwa na ugonjwa wa Corona.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: