MCHORAJI na mwongozaji wa vibonzo au cartoons vya panya (Tom) na
paka (Jerry) Eugene Merrill Deitch amefariki dunia ghafla akiwa na umri wa
miaka 95 huko nyumbani kwake Prague, Na hii ni kwa mjibu wa
mchapishaji wa movie zake Peter Himmel .
Imeelezwa kuwa Eugene aliyezoeleka kuitwa Gene ambaye pia ni mshindi
wa tuzo ya Oscar alifariki dunia ghafla siku ya Alhamisi usiku akiwa katika
makazi yake.
Gene ameongoza sehemu zipatazo kumi na tatu za vibonzo au cartoons
zipendwazo na watoto ulimwenguni kote maarufu kama "Tom and Jerry"
pamoja na baadhi kutoka mfululizo wa visa vya Popeye.
Gene aliwahi kufanya kazi kama msanifu wa anga la Amerika Kaskazini
kabla ya kuajiriwa jeshini na kuingia katika mafunzo ya majaribio ya
urubani na mwaka 1959 alihamia katika makazi yake huko Prague.
Awali Gene alitengeneza mfululizo wa filamu ya visa ya Tom ambapo
Sidney's Family Tree iliteuliwa katika tuzo Academy mwaka 1958.
Aidha filamu yake ya Munro ilishinda tuzo,kitengo cha filamu bora ya picha
na michoro mwaka 1960 na alichaguliwa mara mbili katika uteuzi wa
kipengele cha namna hiyo mwaka 1964 kwa filamu za Nudnik na How to
Avoid Friendship.
Gene alikua akiishi na mkewe na watoto wake wa kiume watatu kutoka
ndoa yake ya kwanza ambao wote ni wahusika katika kuandika na kudirect
au kuongoza vibonzo.
Mashabiki wengi wameeleza kusikitishwa na kifo hicho ambapo kurasa
nyingi za Twitter zimejaa Salamu za rambirambi kufuatia kifo hicho ambapo
wengi wameeleza kuwa Gene alikuwa zaidi ya Tom na Jerry na
atakumbukwa daima kupitia vibonzo hivyo.