Katika hali isiyo ya kawaida mwanaume aliyejulikana kwa jina la Kaido Mfilinge (30)
anayedaiwa kuwa ni mganga wa kienyeji alikutwa amejinyonga mpaka kufa katika mtaa
wa Nazareti mjini Njombe nchini Tanzania
Hii ni baada ya kuchukua dawa kwa mganga mwenzie kutoka mkoa wa Ruvuma
humohumo nchini .Alipokiuka masharti ambayo alikuwa amepewa na mganga akaamua
kuacha ujumbe wa maandishi wa kuomba msamaha kwa mizimu kabla ya kujitia kitanzi.
Na barua aliyoiacha inasema, "Nimejinyonga baada ya kusumbuliwa na kibuyu
ambacho nilikuwa nimepewa na mganga na kusababisha mizimu kuanza kusumbua".
Akizungumza na vyombo vya habari kuhusu tukio hilo kamanda wa jeshi la polisi mkoa
wa Njombe Hamis Issa alisema,
“Huyu kijana yeye ni mganga wa kienyeji kwa asili yake na amejinyonga baada ya
kwenda mkoa wa Ruvuma akapewa dawa iliyokuwa na masharti,ile dawa aliyoenda
nayo nyumbani kwake kibuyu kimoja kikaanza kumsumbua akamuuliza Yule aliyempa
akaambiwa akatupe kwenye njia panda yoyote”,alisema kamanda Hamis Issa
Kamanda Issa ameongeza kuwa “Lakini yule kijana akaamua kuchukua maamuzi
magumu akajinyonga na haya maneno ninayoyaongea ameyaandika mwenyewe
kwenye karatasi yake "Samahani mizimu nimekosea masharti,samahani familia
yangu,samahani mganga wangu uliyenipa masharti nimekosea nimeaamua kujitoa
duniani kwa kujinyonga" na hiyo karatasi ipo imeandikwa hivyo ,alisema Kamanda Issa.