14.6 C
Nairobi
Thursday, August 5, 2021
Kenya
206,691
Total confirmed cases
Updated on August 5, 2021 6:33 am

SARAH OBAMA, BIBI YA RAIS WA ZAMANI BARACK OBAMA AFARIKI DUNIA

Sarah Obama, bibi ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amefariki dunia katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu akiwa na miaka...
More

  Latest Posts

  MGONJWA AFARIKI BAADA YA KUFANYIWA UPASUAJI NA DAKTARI MWENYE VYETI FEKI

  Nyanja ya utabibu imepigwa na mshtuko baada ya kuibuka kuwa afisa mmoja wa kliniki katika Hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Kisii(KTRH)iliyoko nchini Kenya amekuwa akihudumu hospitalini humo kwa miaka minane akitumia vyeti feki.

  Kwa mujibu wa ripoti ya Daily Nation Jumatatu, Februari 8, Katibu Mkuu wa Chama cha Maafisa wa Kliniki nchini(KUCO), George Gibore alisema mshukiwa huyo amekuwa akitumia nambari ya usajili ya daktari mwingine ambaye anahudumu katika kaunti ya Pokot Magharibi.

  Gibore alisema uchunguzi ulianzishwa dhidi ya daktari huyo baada ya kumfanyia mgonjwa upasuaji ambaye baadaye alifariki. Na kumuacha mgonjwa mwingine katika hali mahututi baada ya kumfanyia upasuaji. Rekodi zake zilikaguliwa baada ya kuibuka kwamba alikuwa akifanya kazi usiku wakati maafisa wenzake wa kliniki walikuwa wamegoma.

  Katibu wa Kuco tawi la Kisii, Victor Bwanchete, alianza kumchunguza daktari huyo ambaye alikuwa anafanya kazi usiku wenzake wakishriki mgomo na kubaini ilikuwa kweli.

  Afisa Mkuu wa hospitali hiyo Enock Ondari alisema hakuwa anafahamu suala hilo huku KUCO ikisema suala hilo limeripotiwa kwa polisi na kutaka uongozi wa hospitali hiyo kuelezea namna mshukiwa aliajiriwa.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: