22.8 C
Nairobi
Friday, October 15, 2021
Kenya
251,669
Total confirmed cases
Updated on October 14, 2021 9:34 pm

SARAH OBAMA, BIBI YA RAIS WA ZAMANI BARACK OBAMA AFARIKI DUNIA

Sarah Obama, bibi ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amefariki dunia katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu akiwa na miaka...
More

  Latest Posts

  MIGUNA MIGUNA ATEULIWA KUGOMBEA UGAVANA NAIROBI

  Kwenye taarifa iliyotolewa leo tarehe 28 mwezi Desemba, 2020 na kutiwa saini na Mwenyekiti wa Kitaifa wa chama cha Thirdway Alliance Kenya, Miruru Waweru, chama hicho kimemtangaza Wakili Miguna Miguna kuwania kiti hicho katika uchaguzi mdogo utakaofanyika tarehe 18 mwezi Februari mwaka 2021.

  Miguna Miguna alikuwa mmoja wa wagombea wa Ugavana kupitia kwa chama hicho kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2017 ambapo Mh.Mike Sonko alishinda.

  Wakili huyo mwenye uraia wa nchini Canada kwa sasa yuko Canada baada ya kufurushwa humu nchini kufuatia hatua ya kumuapisha Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga kama Rais wa Watu mnamo mwaka wa 2018.

  Chama cha Thirdway Alliance kimetoa taarifa hiyo Jumatatu, ikiwa ndiyo siku ya mwisho ya vyama kuwasilisha majina ya wanachama waliowateua kushiriki kwenye uchaguzi huo mdogo kwenye kugombea kiti cha Ugavana katika kaunti ya Nairobi kwa Tume ya Uchaguzi na Mipaka, IEBC.

  Kiti cha Ugavana wa Kaunti ya Nairobi kiliachwa wazi baada ya kubanduliwa mamlakani kwa Mh.Mike Mbuvi Sonko kwa tuhuma za ufisadi, miongoni mwa madai mengineyo.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: