16.1 C
Nairobi
Sunday, September 26, 2021
Kenya
248,392
Total confirmed cases
Updated on September 26, 2021 8:39 am

SARAH OBAMA, BIBI YA RAIS WA ZAMANI BARACK OBAMA AFARIKI DUNIA

Sarah Obama, bibi ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amefariki dunia katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu akiwa na miaka...
More

  Latest Posts

  MLIPUKO MKUBWA WA VOLKANO WATOKEA DRC CONGO

  Mlipuko mkubwa wa volkano umeshuhudiwa katika Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo usiku wa kuamkia leo Jumapili Mei 23.

  Mlipuko huo ulitokea kwenye Mlima Nyiragongo ulioko maili sita tu kutoka mji wa Goma ulio na wakazi milioni mbili.

  Mtiririko wa lava ulifika uwanja wa ndege wa jiji hilo lakini imeripotiwa sasa umesimama.

  Mamlaka ya Rwanda ilitangaza kuwa zaidi ya watu 3,000 walivuka mpaka kutoka Goma-DRC na kuingia Rwanda asubuhi ya Jumapili.

  Umati wa wakazi wa Goma-Kongo wakikimbilia Usalama

  Uokoaji ungali unaendelea katika mji huo wa Goma ulio hatarini.

  Hata hivyo,sio mara ya kwanza Mlima Nyiragongo kuwa na mlipuko wa Volkano kwani umewahi kutokea mwaka 1977 ambapo watu zaidi ya 600 walipoteza maisha na wengi kuachwa bila makao.Pia watu 250 walipoteza maisha na 120,000 kuachwa bila makao huko Goma mwaka 2002.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: